NBA: WARRIORS WAWACHABANGA ROCKETS NYUMBANI KWAO, CURRY NA KLAY WAWEKA REKODI MPYA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 15, 2019

NBA: WARRIORS WAWACHABANGA ROCKETS NYUMBANI KWAO, CURRY NA KLAY WAWEKA REKODI MPYA


Moja kati ya michezo ambayo imekuwa ikibeba attention kubwa ya watu wanaofuatilia ligi ya mpira wa kikapu duniani ni kati ya mabingwa watetezi Golden State Warriors Vs Houston Rockets ambao wamedhamiria kuuondoa ubabe wa Warriors katika kanda ya magharibi. 

Timu zote zina wachezaji wa hali ya juu tena waliowahi kuwa wachezaji bora wa ligi hiyo kama Stephen Curry, na James Harden. 

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa timu ya Rockets, Uliisha kwa Rockets kufungwa 106-104 huku mchezaji mpya wa Warriors Demarcus Cousin akiwa nyota wa mchezo huo kwa kufunga pointi 27. 

Katika mchezo huo wachezaji Klay Thompson Pamoja na Stephen Curry waliweka rekodi ya kuwa wachezaji pekee katika historia ya NBA kufunga japo point tatu  katika misimu 7. Hakuna mchezaji mwingine yeyotw katika historia ya NBA aliyewahi kuzidi misimu 5 tu. 


Loading...

No comments: