NDEGE YA SERIKALI KUANZA KAZI, YAPAKWA RANGI KWA MILIONI TANO

Rais John Magufuli amesema ndege ya Serikali aliyoagiza ipelekwe Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kuanza kusafirisha abiria inakamilisha upakaji rangi kwa Sh5 milioni tofauti na Sh260 milioni zilizotajwa na wataalamu.

Rais John Magufuli

Rais Magufuli amesema wataalamu walishauri ndege hiyo ikapakwe rangi, kuandika maneno, na kuchorwa Twiga nje ya nchi wakati jambo hilo linawezekana kufanyika nchini.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam leo Machi 28, 2019  baada ya kupokea taarifa ya Takukuru na kumuapisha Balozi wa Cuba, Valentino Mlowola, Rais Magufuli amesema bado suala la rushwa ni tatizo.

“Nchi hii ni hatari, kuna wajuaji wengi katika nchi hii, kuna maajabu mengi yanafanyika katika nchi hii,” amesema Rais Magufuli.

Akitoa mfano wa ndege, Rais Magufuli amesema aliposema ndege ya hiyo ipelekwe ATCL kuanza kusafirisha abiria, wataalamu walipokea na suala likawa kubadilisha maneno na twiga.

Amesema walimwambia kuwa suala hilo haliwezi kufanyika nchini na kutafutwa nchi tatu ambako, ndege hiyo ingeenda kupakwa rangi.

Ameeleza kuwa  aliwaambia watafute mtu atakayeweza kufanya hivyo lakini walikaa kimya wakidhani amesahau mpaka jumapili moja alipoambiwa ndege hiyo itapelekwa nje.

Rais Magufuli amesema waliotakiwa kusafirisha ndege hiyo walishalipwa Sh60 milioni wakati fedha za matengenezo zilizohitajika zikiwa Sh200 milioni.

Rais Magufuli amesema aliwaambia ndege itakapokuwa inapaa na nafasi zao zitapaa jambo lililofanya ibaki.
“Ndege haikuondoka na imepakwa rangi kwa Sh5 milioni,” amesisitiza.

Rais Magufuli amesema rushwa ni ugonjwa na kwamba hauna chama.

“Rushwa ni mbaya na wanaochukua hawafaidiki, kama rushwa ikipungua nchi hii itafanikiwa siku alipoambiwa kuwa ndege hiyo,”amesisitiza Rais Magufuli.

Amesema fedha zilizookolewa katika mapambano ya rushwa zitatumika kuleta maendeleo ikiwamo kununua dawa na ujenzi wa shule.

Awali  Kamishna wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  Diwai Athmani alisema taasisi hiyo imefanikiwa kuokoa kiasi cha Sh70.3 bilioni ikilinganishwa na Sh14.6 zilizookolewa  mwaka 2016/2017.

Alisema Mbali na fedha hiyo, amesema taasisi hiyo pia imefanikiwa kufungua kesi 495 za rushwa katika kipindi cha mwaka 2017/2018 ikilinganishwa na kesi 435 zilizofunguliwa mahakamani mwaka 2016/2017.

Chanzo:Mwananchi

RAIS MAGUFULI AMWAPISHA VALENTINO MLOWOLA KUWA BALOZI WA TANZANIA CUBA

Post a Comment

0 Comments