Ndoa yafungwa wodini baada ya bwana harusi kushambuliwa na kulazwa - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 13, 2019

Ndoa yafungwa wodini baada ya bwana harusi kushambuliwa na kulazwaWanandoa Muneer Hercules na Maryam Kallile wameweka historia kwenye hospitali ya Gatesville Melomed nchini Afrika Kusini kwa kuwa wanandoa wa kwanza kufunga ndoa kwenye wodi za hospitali hiyo kufuatia sherehe iliyofanyika Jumapili Machi 10.

Wawili hao walilazimika kufunga ndoa hiyo baada ya Muneer kushambuliwa na majambazi siku ya Jumamosi akiwa nyumbani kwenye jiji la Cape Town na kujeruhiwa hali iliyopelekea kulazwa hospitalini siku moja kabla ya siku ya kufunga ndoa.

Iliulazimu uongozi wa hospitali hiyo kuruhusu ndoa hiyo ifungwe kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Muneer baada ya kukisaficha chumba hicho na kuwaruhusu watu wachache wa karibu na familia hiyo kusherehekea kidogo bila kuathiri utaratibu wa hospitali.

Hercules ameruhusiwa kutoka hospitalini mapema hii leo baada ya hali yake kuimarika.
Loading...

No comments: