NI BARCELONA Vs JUVENTUS KATIKA KUIPATA SAINI YA BEKI MATTHIJS DE LIGT - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

NI BARCELONA Vs JUVENTUS KATIKA KUIPATA SAINI YA BEKI MATTHIJS DE LIGT


Mabingwa watetezi wa Serie A, klabu ya Juventus,  wameingia vitani dhidi ya Barcelona kuwania saini ya beki wa Kidachi kutoka klabu ya Ajax aitwaye Matthijs de Ligt. 

De Ligt ambaye pia anawindwa sana na mabingwa watetezi wa LALIGA, klabu ya FC Barcelona, ambao wapo tayari kumuuza beki wao Mfaransa Samuel Umtiti majira ya kiangazi na timu za jiji la Manchester zimeshaanza kuonyesha nia.

Taarifa zinasema kuwa kama Juventus watashindwa kumnasa Matthijs de Ligt, basi watahamishia nguvu zao zote kwa beki wa Benfica Ruben Dias na beki wa Atletico Madrid Stefan Savic. 

SOURCE: Tuttosport
Loading...

No comments: