PAPA FRANCIS AZUNGUMZIA SAKATA WA PETE YAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 29, 2019

PAPA FRANCIS AZUNGUMZIA SAKATA WA PETE YAKE

Papa Francis amevunja ukimya juu ya mkasa wa kuzuia waumini kubusu pete yake akisema lilikuwa ni suala la kiafya zaidi.Msemaji wa Vatican Alessandro Gisotti amesema kuwa Papa alikuwa akihofia kusambaa kwa vijidudu alipokuwa akikutana na waumini wa Kanisa Katoliki siku ya Jumatano.Wahafidhina ndani ya kanisa walipinga vikali kitendo hicho wakidai Papa anavunja utamaduni wa muda mrefu wa kanisa.

"Lilikuwa tu ni suala la kiafya," Bwana Gisotti amesema siku ya Alhamisi, akiwaambia maripota kuwa yeye mwenyewe alimuuliza Papa juu ya suala hilo.

Gisotti amesema kuwa kulikuwa na watu wengi waliokuwa kwenye msururu wa kumsalimia Papa na yeye akawa na tahadhari juu ya uwezekano wa kusambaza vijidudu.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki mwenye miaka 82 anadaiwa kuwa "kufurahishwa" na utata huo, msaidizi wa Papa ameliambia shirika la habari la Reuters.

"Papa anapenda kuwakarimu watu, na yeye pia hupenda kukarimiwa", amesema Gisotti na kuongeza kuwa Papa hufurahia kuwaruhusu watu kwenye makundi madogo kubusu pete yake.

Pete ya Papa, inayovaliwa kwenye kidole cha kati cha mkono wa kulia ndiyo alama yenye nguvu zaidi ya utawala wa Papa.

Kubusu pete hiyo - ni utamaduni ulioasisiwa miongo mingi iliyopita - inachukuliwa kama alama ya heshima na utii kwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki.

Mara tu baada ya Papa kufariki, pete yake mara moja huteketezwa ikiwa ni kiashiria kuwa utawala wake umefikia kikomo.

Chanzo: BBC Swahili
Loading...

No comments: