PEP GUARDIOLA AWATAKA WACHEZAJI WAKE WASIWE NA MAJUTO IWAPO WATASHINDWA KUWA MABINGWA WA EPL MSIMU HUU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

PEP GUARDIOLA AWATAKA WACHEZAJI WAKE WASIWE NA MAJUTO IWAPO WATASHINDWA KUWA MABINGWA WA EPL MSIMU HUU


Kocha wa klabu ya Mancester City, Mhispania Pep Guardiola amesema kwamba wachezaji wa Manchester City hawatakiwi kuwa na majuto endapo wakishindwa kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Uingereza na taji hilo kwenda Liverpool. 

Guardiola anaamini kwamba timu yake sasa hivi inacheza soka bora sana kuliko msimu uliopita ambao walivunja rekodi ya pointi katika ligi hiyo. 

"Kwa jinsi tunavyocheza, ni bora zaidi ya msimu uliopita. Kila mtu anajua nini tunachotakiwa kufanya. Kila mtu anamsaidia mwenzake. Na pindi hiyo ikitokea tunaweza kushindana, na kama tukipoteza basi tumepoteza hakuna majuto"

"Najua kwenye jamii yetu wa kwanza ndio anapewa pongezi zaidi na wa pili hana maana yoyote. Lakini haiwezekani hiyo mimi kujisikia hivyo kuhusu wachezaji wangu. Haiwezekani" Alimalizia kocha huyo ambaye tayari ameshachukua kikombe kimoja msimu huu cha CARABAO na anategemewa kuchukua ligi kuu na hata Uefa Champions League kutokana na ubora na upana wa kikosi chake. 
Loading...

No comments: