Picha: Msanii Young Killer afungua Studio yake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 13, 2019

Picha: Msanii Young Killer afungua Studio yake
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Young Killer amefanikiwa kufungua studio yake binafsi.

Rapa huyo kutokea mkoani Mwanza ambaye anafanya vizuri na ngoma 'Secreto' ameeleza kuwa hiyo ilikuwa ni ndoto yake kwa mwaka huu.

"Moja ya ndoto zangu kwa mwaka 2019 ilikuwa ni pamoja na kuwa na studio yangu binafsi nyumbani kwangu, nashukuru Mungu ameniwezesha," ameeleza Young Killer.

Miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wenye studio ambazo zimekuwa zikifanya vizuri ni pamoja na Diamond Platnumz, Nay wa Mitego na Quick Rocker.
Loading...

No comments: