Pinda ampokea Mwenyekiti wa Bavicha aliyetimkia CCM na wanachama 233 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 22, 2019

Pinda ampokea Mwenyekiti wa Bavicha aliyetimkia CCM na wanachama 233


Mizengo Pinda ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, amewapokea wanachama wapya wa upinzani 233 akiwemo mwenyekiti wa vijana (Bavicha) Mkoa wa Manyara, Frank Oleleshwa na aliyekuwa Katibu wa Chadema wilayani Simanjiro.
Wamepatiwa kadi za CCM na Pinda katika ziara yake ya siku nane Mkoa wa Manyara.
Akizungumza leo kwa niaba ya wanachama wenzake, Oleleshwa amesema sababu za kuhamia CCM zipo nyingi ila yale aliyokuwa anapigania alipokuwa Chadema yanafanyika CCM.
"CCM imeonyesha utashi mkubwa wa uzalendo katika kuongoza nchi hivyo tumeamua kuhamia huku ili kuunga mkono juhudi hizo," amesema Oleleshwa.
Akizungumza baada ya kuwakabidhi kadi wanachama hao wapya wa sehemu mbalimbali wilayani Simanjiro, Pinda aliwapongeza kwa kujiunga na CCM.
Pinda amesema hivi sasa Rais Magufuli anafanya kazi kubwa ya kufanikisha maendeleo hivyo Watanzania wanapaswa kumuunga mkono.
Loading...

No comments: