Profesa Nathan Alexander asifiwa kwa kufundisha huku amembeba mtoto wa mwanafunzi wake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 5, 2019

Profesa Nathan Alexander asifiwa kwa kufundisha huku amembeba mtoto wa mwanafunzi wake

Professor Nathan Alexander hold baby Assata
Twitter/@Original_Vaughn
Profesa Nathan Alexander anasema mtoto huyo kwa jina la Assata alikuwa ametulia sana alipombeba


Profesa mmoja wa hesabu nchini Marekani amepokea sifa nyingi mara baada ya picha yake akiwa amembeba mtoto wa mwanafunzi wake akiwa anafundisha darasani, kusambaa mitandaoni. 
Mtoto huyo Assata alikuwa amekuja darasani na baba yake, Wayne Hayer, ambaye alikuwa amekosa mtu wa kumsaidia kumlea mtoto huyo nyumbani.
Mara baada ya mwanafunzi huyo kuelezea hali iliyomkuta kwa Profesa Nathan Alexander, mwalimu huyo aliamua kumbeba mtoto huyo kwa muda wa dakika 50 wa kipindi chake chote kwa nia ya kumpa fursa mwanafunzi wake Hayer kuandika dondoo ya kile alichokuwa anakifundisha.

"Sijabahatika kuwa na mtoto hivyo hata wakati nambeba mtoto huyu nilikuwa nna hofu kuwa atalia, lakini cha ajabu ni kuwa alikuwa ametulia vizuri sana".
Profesa Alexander anafundisha katika darasa la wanaume lililoko kwenye chuo cha kihistoria cha watu weusi huko Atlanta, Georgia.
Profesa Alexander mwenye umri wa miaka 34, aliripotiwa akimwambia mwanafunzi wake Hayer kuwa anaweza kuwa anamleta mtoto wake darasani kila siku mara baada ya kugundua kuwa mwanafunzi huyo huwa anawahi kutoka ili kuwahi kumlea mtoto wake.
Profesa Alexander alipohojiwa na chombo cha habari cha Marekani cha CNN, alisema "Huyu mwanafunzi huwa ana kazi mbili nazo ni kuhudhuria kusoma siku nzima na kuwa mzazi na mlezi".


SOMA ZAIDI HAPA 
Loading...

No comments: