R Kelly Kurudishwa Tena Rumande - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 7, 2019

R Kelly Kurudishwa Tena Rumande


R Kelly Kurudishwa Tena Rumande
Jaji mmoja mjini Chicago Marekani ameamuru mwanamuziki wa R&B R. Kelly, asalie rumande hadi pale atakapo lipa gharama ya malezi ya kima cha dola $161,000 kwa mke wake wa awali bi Andrea Kelly na watoto wao watatu.

Hivi karibuni nyota wa miondoko ya R&B R Kelly alionyesha masikitiko yake dhidi ya shutuma za unyanyasaji wa kingono zinazomkabili, katika kipindi kimoja cha asubuhi cha televisheni.

Ikiwa ni mara ya kwanza mwanamuziki huyo kuhojiwa tangu akamatwe na polisi mwezi uliopita alisema,"Sijafanya vitu hivyo, huyo sio mimi " na kusisitiza kuwa anapambania maisha yake.

Mwendesha mashitaka wa Chicago alimfungulia Kelly mashtaka 10 yanayohusiana na makosa ya unyanyasaji wa kingono, huku yakihusisha waathirika wanne ambao watatu kati hao walifanyiwa unyanyasaji wakiwa na umri chini ya miaka 18 .
Loading...

No comments: