RAGE: MAZEMBE YA SASA NI JINA TU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 22, 2019

RAGE: MAZEMBE YA SASA NI JINA TU


Baada ya Simba kupangwa kucheza na TP Mazembe katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Ismail Aden Rage, amesema Mazembe kwa sasa ni jina tu.

Rage ameeleza kuwa Mazembe kali aliyokuwa anaifahamu ni ile iliyokuwa na wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu na si hii ya sasa.

Amesema kipindi ina watanzania hao wawili ilikuwa na moto wa kuotea mbali tofauti na ya sasa ambayo itakuwa mchekea kwa Simba.

"Niwaondoe hofu wanasimba wote, Mazembe ya sasa imebaki jina tu.

"Mazembe iliyokuwa na Samatta pamoja na Ulimwengu ndiyo ilikuwa na balaa lake.

"Hivyo Simba tunapaswa nafasi ya kufuzu kwenda nusu fainali, kwangu naamini tutashinda wala hakuna wasiwasi".

Simba itakutana na Mazembe Aprili 5/6 katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam na baadaye Simba watasafiri kuelekea Lubumbashi kurudiana nao 12/13 Aprili huko Congo.
Loading...

No comments: