Rais Magufuli afanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 17, 2019

Rais Magufuli afanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Machi, 2019 amekutana na Mjumbe Maalum wa Rais ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Mhe. Sam Kutesa aliyewasilisha ujumbe kutoka kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni .

Baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mjumbe huyo Sam Kutesa amesema pamoja na kuwasilisha barua kutoka kwa Rais Museveni amezungumza na Rais Magufuli kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri na wa kidugu uliopo kati ya Tanzania na Uganda .

Ameongeza kuwa Rais Magufuli amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa za kwenda nchini Uganda na ametaja baadhi ya juhudi hizo kuwa ni kuimarisha reli ya kati, kukarabati mabehewa 400 ambapo 50 kati yake yamekamilika na kwamba ni matumaini kuwa juhudi hizo zitawawezesha wafanyabiashara wa Uganda kusafirisha mizigo yao bila kikwazo.
Loading...

No comments: