RAIS MAGUFULI AMWAPISHA VALENTINO MLOWOLA KUWA BALOZI WA TANZANIA CUBA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

RAIS MAGUFULI AMWAPISHA VALENTINO MLOWOLA KUWA BALOZI WA TANZANIA CUBA

Rais John Magufuli amemwapisha Kamishna Valentino Mlowola kuwa balozi mpya wa Tanzania nchini Cuba.

Balozi Valentino Mlowola

Kazi ya kumwapisha Balozi Mlowola imefanyika leo Alhamis Machi 28, Ikulu jijini Dar es Salaam ikiambatana na shughuli ya kupokea taarifa ya utendaji kazi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Akizungumza baada ya kuapishwa, Balozi Mlowola amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua na kumuonyesha imani katika kuwatumikia Watanzania.

Amesema anafahamu malengo ya Serikali na dhamira aliyonayo Rais Magufuli ya kuendeleza nchi katika nyanja ya kiuchumi na amani kiujumla.

“Lakini pia nafahamu matarajio ya wananchi wa Tanzania katika kuhakikisha wanapata maisha bora zaidi,” amesema.

Akiongea baada ya kumuapisha Rais Magufuli amtaka Balozi Valentino Mlowola akaanze kazi  mara moja nchini Cuba.

"Nakuomba Valentino Mlowola nimekuteua,uende Cuba.Kuna Balozi wa Zambia nimemteua,kila siku nawaona anazunguka kwenye ofisi anaaga.Mara kwa Waziri Mkuu,Mara Makamu wa Rais,mara Zanzibar.Mwache aendelee kuaga, akimaliza kuaga,ubalozi atakuwa hana"


Pia Rais Magufuli amemtaka Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Valentino Mlowola kwenda na mke wake ili akawe msaidizi wake huko. Rais amemwagiza Waziri wa Mambo ya Nje kumwamisha kikazi mke balozi huyo kama ni mtumishi wa umma, akafanye kazi nchini Cuba.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi amesema atamkabidhi balozi huyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kutekeleza majukumu yake.


NDEGE YA SERIKALI KUANZA KAZI, YAPAKWA RANGI KWA MILIONITANO
Loading...

No comments: