Rais Magufuli atoa ndege ajili ya kusafirisha mwili wa Ruge Mutahaba - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

Rais Magufuli atoa ndege ajili ya kusafirisha mwili wa Ruge Mutahaba


Rais Magufuli atoa ndege ajili ya kusafirisha mwili wa Ruge Mutahaba

Kwa mujibu wa Msemaji wa familia ya Mutahaba, Ndg. Kashasha, Rais Magufuli ametoa ndege kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu Ruge Mutahaba na waombolezaji siku ya Jumapili kwenda Bukoba atapozikwa.

Mwili wa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba utawasili leo saa 9:00 Alasiri kutoka nchini Afrika Kusini.

Pia utakumbuka November mwaka jana Rais John Magufuli alitoa dola za Marekani 20,000 kwaajili ya matibabu ya Ruge.

Ruge Mutahaba atazikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya Jumatatu, siku ya Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba.

Ruge Mutahaba amefariki siku ya February 26 mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.
Loading...

No comments: