IRAN YAITUHUMU MAREKANI KUTAKA KUIPINDUA NCHI HIYO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 7, 2019

IRAN YAITUHUMU MAREKANI KUTAKA KUIPINDUA NCHI HIYO


Rais wa Iran Hassan Rouhani ameituhumu Marekani kwa kupanga njama ya kutumia shinikizo la kiuchumi kuipindua serikali ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu, na kufuta uwezekano wa kufanya mazungumzo na Marekani. 

Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa kwenye mkoa wa kaskazini wa Gilan, Rouhani amesema Iran haiko katika vita vya kiuchumi na kisaikolojia na Marekani na washirika wake. 

Mvutano kati ya Marekani ulianza upya baada ya Rais Donald Trump kuiondoa Marekani kutoka kwa makubaliano ya mwaka wa 2015 yaliyofikiwa kati ya mataifa yenye nguvu duniani na Iran ambayo yalidhibiti shughuli zake zenye utata za nyuklia. 

Trump alisema makubaliano hayo yalikuwa na mapungufu kwa sababu hayakudhibiti mpango wa Iran wa makombora ya masafa marefu au msaada kwa washirika wake nchini Syria, Lebanon, Yemen na Iraq. 

Marekani ilirejesha vikwazo dhidi ya Iran ambavyo vilikuwa vimeondolewa mwaka wa 2016 kufuatia mkataba huo.

CHANZO: DW
Loading...

No comments: