Rais wa Zanzibar Aipongeza Taifa Starts kwa Ushindi - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

Rais wa Zanzibar Aipongeza Taifa Starts kwa Ushindi


Rais wa Zanzibar Aipongeza Taifa Starts kwa Ushindi
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameipongeza timu ya soka ya taifa, Taifa Stars kwa kuifunga Uganda na kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika Afcon 2019.

Stars imefuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.

Katika salamu zake hizo za pongezi, Rais Shein alisema wananchi wa Zanzibar na Tanzania nzima wamefarijika na ushindi huo ambao utaendelea kuipa hadhi kubwa Tanzania Kitaifa na Kimataifa katika anga za michezo.

Alieleza kuwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania nzima wataendelea kuiunga mkono Timu yao hiyo kutokana na jitihada kubwa inazozichukua katika kuhakikisha inailetea ushindi Tanzania.

Aidha, Rais Shein alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wote kwa kuishangilia timu yao.

Alilipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kocha mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, watendaji na viongozi wote waliofanikisha ushindi huo kwa kuonesha kiwango cha hali ya juu. 
Loading...

No comments: