RASMI SASA, FC BAYERN WAMSAJILI BEKI LUCAS HERNANDEZ KUTOKA ATLETICO MADRID - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

RASMI SASA, FC BAYERN WAMSAJILI BEKI LUCAS HERNANDEZ KUTOKA ATLETICO MADRID


Mabingwa wa Bundesliga, klabu ya Bayern Munich wametangaza usajili wa beki raia wa Ufaransa Lucas Hernandez kutoka Atletico Madrid kwa mkataba wa miaka mitano kuanzia Julai Mosi kwa ada ya Euro Milioni 80.

Lucas Hernandez alikuwa mchezaji wa Atletico Madrid na aliisaidia klabu hiyo kutwaa taji la Europa msimu uliopita.

Kuondoka kwa Lucas ni mwanzo tu kwani wachezaji wengine wa Atletico kama Antoinne Griezmann, Filipe Luiz, na Saul Niguez wamehusishwa na kusajiliwa katika dirisha kubwa la usajili litakalofunguliwa mnamo mwezi julai.

Loading...

No comments: