RASMI: SERGIO RAMOS AFUNGIWA KUCHEZA MECHI MBILI ZA ULAYA. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

RASMI: SERGIO RAMOS AFUNGIWA KUCHEZA MECHI MBILI ZA ULAYA.


Kapteni wa klabu ya Real Madrid nchini Hispania, Sergio Ramos amepewa adhabu na shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) ya kusimamishwa kucheza mechi 2 kwa kosa la kujipatisha kadi ya njano katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Ajax. 

Beki huyo wa kati wa washindi mara 3 mfululizo wa ligi ya mabingwa Ulaya, Real Madrid, alipewa kadi hiyo dakika ya 89 katika mechi iliyoisha kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ajax katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ili aukose mchezo wa marudiano pale Santiago Bernabeu. 

Ramos amepata alichokuwa anakitaka lakini pia ataukosa mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali iwapo Real Madrid itaishinda Ajax na kusonga mbele. 

Loading...

No comments: