RUNGU LA TFF LAWAKUTA YANGA, SIMBA, NA ABDALLAH SHAIBU 'NINJA' - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 11, 2019

RUNGU LA TFF LAWAKUTA YANGA, SIMBA, NA ABDALLAH SHAIBU 'NINJA'


KLABU ya Simba imetozwa faini ya milioni tatu kwa kuingia uwanjani wakitumia mlango usio rasmi, lakini vilevile kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea . Adhabu imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo 

Vilevile klabu ya Yanga imetozwa faini ya milioni sita kwa makosa mawili; moja ni kuingia uwanjani wakitumia mlango usio rasmi na lingine ni kosa la kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji kukaguliwa wakiwa koridoni badala ya vyumbani. 

Ukiachana na adhabu/faini hizo za watani wa jadi, mchezaji beki wa Yanga, Abdallah Shaibu Ninja amefungiwa na kamati ya nidhamu ya TFF mechi 3 kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union. 

Loading...

No comments: