Samatta Aipongeza TFF, Afuta ‘Tweet’ Ya Awali - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

Samatta Aipongeza TFF, Afuta ‘Tweet’ Ya Awali

Ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh John Magufuli kutangaza kuwazawadia viwanja wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2019.Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa mipango ya kuwazingatia wachezaji wote wa walioshikiri katika harakati za kufanikisha timu kufuzu kwenye AFCON 2019.

Kupitia ukurasa wake wa kwenye mtandao wa twitter, Samatta ameandika “

Tuwapongeze shirikisho mpira wa miguu Tanzania kwani linamipango na wachezaji wote walioshiriki katika kampeni hii ya kuwania tiketi na kwa heshima yao basi naondoa Twitte yangu iliyopita kwani tayar mipango ipo barabara kwa kila mchezaji aliyeshiriki. asanteni tff🙏”

Awali kabla ya tweet hiyo, Samatta  ali tweet  akiomba mchezaji Shomari Kapombe apewe zawadi kama wachezaji wengine wa Taifa Stars.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Samatta aliandika "Kama Kapten ningeomba TFF imuangalie Shomari Kapombe katika zawadi ambazo wachezaji watapata. Ikishindikana basi ningeomba wachezaji wote tumchangie kidogo kidogo".

Aliongeza "Endapo vyote visipowezekana kabisa basi katika ahadi ya Mh Paul Makonda, nitagawana naye nusu kwa nusu".

Mh. Paul Makonda na kamati yake ya 'Saidia Taifa Stars ishinde', waliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kila mchezaji wa timu ya taifa endapo watafuzu AFCON jambo ambalo limetimia.

Kapombe alipata majeraha akiwa mazoezini Afrika Kusini siku chache kabla ya kuwakabili Lesotho Novemba 18, 2018.

SAMATTA: NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA NA KAPTENI WA TIMU YANGU YA TAIFA
Loading...

No comments: