SAMATTA: NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA NA KAPTENI WA TIMU YANGU YA TAIFA - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 25, 2019

SAMATTA: NAJIVUNIA KUWA MTANZANIA NA KAPTENI WA TIMU YANGU YA TAIFA

Baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuandika historia kubwa kwenye Uwanja wa Taifa usiku wa jana machi 24, kwa kuifunga timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes" kwa mabao 3-0 na kufuzu kwenye Mataifa ya Afrika AFCON baada ya miaka 39.

Mbwana Samatta
Mchezaji wa kimataifa na nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye aliongoza wachezaji wenzake katika kupata ushindi huo amejivunia kiwango cha juu kilichooneshwa na wachezaji wenzake, uwepo wa mashabiki.

 “Najivunia ubora uliooneshwa na wachezaji wenzangu,najivunia uwepo wa benchi la ufundi likiongozwa na kocha amunike, najivunia uwepo wa mashabiki waliojitokeza kutusapoti katika mchezo wetu wa jana na najivunia kuwa mtanzania na kapteni wa timu yangu ya taifa. Asanteni wote mliohamasisha na wote mliojotokeza kutusapoti 🙏🙏”. Samatta ameandika hayo kwenye ukurasa wake Instagram.

Samatta alikwea pipa usiku wa jana kurudi nchini Ubelgiji katika klabu yake ya Genk.

Taifa Stars imeungana na timu ya taifa ya Uganda, Kenya na Burundi zitakazoiwakilisha Afrika Mashariki katika michuano ya AFCON itakayofanyika kuanzia mwezi June hadi Julai, 2019 nchini Misri.

#BREAKING; RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS NA BONDIA MWAKINYO
Loading...

No comments: