Serengeti Boys watua Uturuki kujiandaa na AFCON-U17


Serengeti Boys watua Uturuki kujiandaa na AFCON-U17
Timu ya Taifa ya vijana (Serengeti boys) tayari imewasili nchini Uturuki kushiriki mashindano ya kimataifa ya UEFA Assist chini ya miaka 17 yanayotaraji kuanza hivi karibuni.

Serengeti Boys wapo Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na Fainali za Afrika kwa Vijana U17 (AFCON), Fainali zitakazofanyika April mwaka huu Tanzania ikiwa mwenyeji.

Utakumbuka February 14 mwaka huu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe alizindua nembo maalumu ya Fainali za Afrika za Vijana chini ya miaka 17 (AFCON-U17).

Post a Comment

0 Comments