SHABIKI WA MAN UNITED APIGWA KISU KWA KUSHANGILIA KUIFUNGA PSG JIJINI PARIS - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

SHABIKI WA MAN UNITED APIGWA KISU KWA KUSHANGILIA KUIFUNGA PSG JIJINI PARIS


Shabiki mmoja wa klabu ya Manchester United amefanyiwa upasuaji wa dharura jijini Paris mara baada ya kuchomwa kisu kifuani na dereva Taxi mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya PSG na MAN UNITED siku ya Jumatano. 

Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 44 alikuwa anarudi katikati ya jiji baada ya mechi na mashabiki wenzake watatu huku wakishangilia mno ushindi huo na ndio hapo dereva huyo alipochukia. 

SkySport imeambiwa kwamba dereva huyo alisimamisha gari na kuwaambia washuke kabla ya kutoa kisu na kumtishia shabiki mwanamke kati ya mashabiki hao watatu. 

Wakati tukio hilo likiendelea, mhanga alijaribu kuingilia kati kumtetea mwanamke lakini dereva akageuzia kisu kwake na kumchoma kifuani ambapo imeelezwa kuwa jeraha ni kubwa sana. 

Shabiki huyo wa United aliwahishwa haraka sana katika hospitali ya Europeen Georges-Pompidou na jana mchana alifanyiwa upasuaji wa kuondoa damu kwenye mapafu yake. 

SkySports wameambiwa kwamba mtuhumiwa amekamatwa leo kuhusiana na shambulio hilo lakini silaha iliyotumika haijapatikana. 

No comments: