Shaka:Taifa linathamini Mchango wa Wanawake - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 9, 2019

Shaka:Taifa linathamini Mchango wa Wanawake

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka amesema taifa lolote lisilothamini mchango wa wanawake ni  butu, dhana ya usawa wa kijinsia ni  kichocheo  cha ushiriki na ushirikishwaji katika maendeleo endelevu ya kila Taifa linalothimini na kujali mchango wa kina mama.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka akiwa moja ya Banda la wajawasiliamari waliohudhuria katika Uwanja wa Jamhuri,Mkoani Morogoro katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Mwanamke Duniani.

 Anasema baba wa Familia ya watanzania  Rais John  Magufuli  alisema  kuwa  serikali anayoiyongoza inathamini kazi nzuri inayofanywa na akina mama, amewataka kuendelee kutembea kifua mbele.

"Nasi wasaidizi wake katika Chama cha Mapinduzi  tunamuunga mkono kwenye hilo ninawahakikishia tutawapa kila aina ushirikiano,  msaada na tutawashika mkono wanawake wa Morogoro na watanzania kwa ujumla  ili muweze kufikia ndoto zenu," anasema

Anasema  ilani ya CCM  2015-2020 imetuelekeza kusimamia na kuendeleza harakati za maendeleo ya wanawake  kiuchumi, kijamii na kisiasa nchini.Loading...

No comments: