SIMBA MAWINDONI KUMPATA PACHA WA KAGERE, TUYISENGE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

SIMBA MAWINDONI KUMPATA PACHA WA KAGERE, TUYISENGE


Katika moja ya Ukurasa wa instagram unaosemekana kuwa wa mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu ya Simba na mjumbe wa bodi kuu ya klabu hiyo, Zacharia Hanspope, kumewekwa picha ya mchezaji huyo akishuka katika basi la timu ya taifa ya Rwanda huku picha hiyo ikiwa na maandishi (caption) "NA BADO".

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Rwanda na klabu ya Gor Mahia ya Kenya, Jacques Tuyisenge tetesi zinasema yuko mbioni kujiunga na mabingwa wa Ligi kuu Soka Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba. 

Je, Tuyisenge akisajiliwa na simba atawika kama anavyofanya aliyekuwa pacha wake Meddy Kagere? 
Loading...

No comments: