Slack imeboresha kitu na kuzidi kuvutia - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

Slack imeboresha kitu na kuzidi kuvutia
Inapotokea mtu/kampuni iliyotengeneza programu fulani halafu ikawa inatoa masasisho baada ya kipindi kupita lazima iwepo sababu iliyosababisha jambo hilo kufanyika vivyo hivyo Slack imeboresha kitu muhimu.

Siwezi kushangaa iwapo mtu atasema kuwa hajawahi kujua/kusikia kuwa kuna programu iitwayo “Slack” ambayo inafanya kazi kwenye simu kama programu tumishi lakini pia kupitia kompyuta kupitia tovuti.

Slack ni nini?

Kwa kazi zinazojumuisha mawasilaino ya watu wengi/kampuni au taasisi na hawapendi kutumia maandishi kwenye karatasi mtakuwa mmeshaambiwa mtumie stack kufanya mawasiliano ya kiofisi.

Slack ni programu tumishi/tovuti ambayo inawezesha kundi fulani kwenye taasisi, kampuni, n.k kuweza kutoa mrejesho, kuuliza swali, kuchangia mawazo pamoja na mengineyo na wengine waliopo kwenye mfumo huo kuweza kusoma ulichokiandika.

Slack imeboresha kitu
Mazungumzo ya watu kwenye Slack ambao wanatika kwenye jumuiya/kampuni moja.

Kitu kipya kwenye Slack.

Taarifa fupi fupi za kumhusu mhusika ni kitu muhimu hasa kutokana na majukumu mbalimbali au maudhui ya programu yenyewe ilivyotengenezwa. Sasa kilichoboreshwa ni kuweka muda ambao utakuwa unafanya kitu fulani; inaweza kuwa leo, kwa dakika 30, saa nzima, n.kBaada ya muda huo kupita taarifa hiyo inapotea/kufutika.
Slack imeboresha kitu
Hicho ndio kilichoreshwa kwenye Slack.

Iwapo ninyi kama kikundi/kampuni hamjawahi kutumia Slack kupitia simu rurunu/kompyuta unaweza kuipakuwa kutoka App Store/Playstore mfurahie mengi zaidi kutoka huko.

Vyanzo: The Verge, Appcues
Loading...

No comments: