S.W.R: LIVERPOOL WAANGUKIA PUA, CITY WARUDI KILELENI, BARCA MBABE WA MADRID MARA NYINGINE, KAMA UTANI BAYERN WAWAFIKIA DORTMUND, MBAPPE HASHIKIKI UFARANSA, BALOTELI ASHANGILIA GOLI KWA SELFIE, JUVE HAWAKAMATIKI, PORTLAND WASHINDA MECHI 6 KATI YA 7... - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

S.W.R: LIVERPOOL WAANGUKIA PUA, CITY WARUDI KILELENI, BARCA MBABE WA MADRID MARA NYINGINE, KAMA UTANI BAYERN WAWAFIKIA DORTMUND, MBAPPE HASHIKIKI UFARANSA, BALOTELI ASHANGILIA GOLI KWA SELFIE, JUVE HAWAKAMATIKI, PORTLAND WASHINDA MECHI 6 KATI YA 7...


1. LIVERPOOL WABANWA NA EVERTON, CITY WARUDI KILELENI RASMI: 
Katika mambo ambayo mashabiki wa Liverpool hawataki kuyasikia kabisa ni matokeo ya mechi yao ya jana dhidi ya mahasimu wao kutoka mji mmoja wa MERSEYSIDE, timu ya Everton. Mechi hiyo iliisha kwa matokeo ya sare tasa 0-0 na kuwaudhi sana mashabiki wa Liverpool ambao walihitaji matokeo sana katika mechi hiyo ili kuendelea kuongoza ligi na kuukaribia ubingwa wa ligi kuu Uingereza. 


Kwa matokeo hayo, Liverpool wameshuka rasmi hadi nafasi ya 2 wakiwa na point 70 huku Manchester City wakiongoza ligi kwa pointi 71 baada ya kushinda mechi yao ya jumamosi 1-0 dhidi ya FC Bournermouth. 


2. BARCA WAENDELEZA UBABE KWA  MADRID BERNABEU:
Wiki iliyopita imeshuhudia mechi kubwa na inayofuatiliwa zaidi duniani ya EL CLASSICO. Siku zote dunia huwa inagawanyika vipande viwili ikifikia mechi hii. Either ushabikie Barcelona au Madrid. Wiki iliyopita jumatano katika mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya kombe la Copa Del Rey uliochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Madrid, SANTIAGO BERNABEU, tulishuhudia Madrid akipokea kichapo cha 3-0 huku wao wakiutawala mchezo kuliko Barcelona. Luis Suarez alihusika katika magoli mawili na moja Verane alijifunga. 


Jumamosi timu hizi mbili kubwa barani Ulaya zikakutana tena katika mchezo wa ligi katika uwanja ule ule wa Real Madrid na goli la mapema kipindi cha kwanza la kiungo Mcroatia IVAN RAKITIC liliweza kuwapa Barca ushindi katika mechi hiyo wa 1-0 na kuitupilia mbali Real Madrid katika mbio za Ubingwa wa ligi kuu ya Hispania, LALIGA. Huo ulikuwa ni ushindi wa 4 mfululizo wa Barcelona katika uwanja wa Santiago Bernabeu. Je Bernabeu imegeuka kuwa ni uwanja wa mazoezi wa Fc Barcelona? 

3. "Kutangulia sio kufika" ndio msemo mashabiki wa Fc Bayern Munich wanautumia sana wiki hii mara baada ya kuwafikia vinara Borussia Dortmund kwa pointi 54 huku wakiachwa kwa tofauti ya magoli tu. Hapo nyuma, Bayern hawakuanza msimu vizuri na waliachwa hadi point 16 na Dortmund. Lakini kupatikana kwa matokeo mabovu kwa Dortmund na kufanya vizuri kwa Bayern sasa hivi kumefanya upepo ubadilike. Dortmund wakiukosa huu ubingwa wajilaumu wenyewe kwani walikuwa na kila sababu na form nzuri ya kuutwaa. 4. YANGA NA SIMBA ZAENDELEA KUFANYA VIZURI LIGI KUU TANZANIA BARA: 
Timu za Yanga na Simba zimeendelea kuufukuzia Ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa kuendelea kushinda mechi zao za wikiendi. Siku ya Jumamosi Yanga walikuwa CCM KIRUMBA kuwakabili timu ya Alliance na waliibuka na ushindi wa 1-0 wa goli la Hamis Tambwe dakika ya 75. Wapinzania wao, Simba Sports Club jana jumapili walikuwa wakipambana na Stand United na walishinda 2-0, magoli ya John Bocco dakika ya 52 na 66. Vita ya Ubingwa bado ni mbichi. Nnai ataibuka bingwa? 5. JUVENTUS HAWAKAMATIKI ITALIA:
Juventus wameendelea kufanya vizuri katika ligi kuu ya Italia maarufu kama SERIE A mara baada ya jana kumfunga mpinzani wake anayemfunguza kwenye mbio za ubingwa timu ya NAPOLI kwa magoli 2-1. Magoli ya Mirem Pjanic pamoja na Emre Can yalitosha kuwakatisha tamaa Napoli na kujikita kileleni zaidi. Juventus wanaongoza ligi sasa kwa pointi 72 huku wanayemfuatia ni Napoli mwenye pointi 56. Je, mbio za Ubingwa Italia zimeisha? 


6. Kylian Mbappe ameendelea kung'aa katika ligi kuu ya Ufaransa na timu yake ya PSG mara baada ya wikiendi hii kufunga magoli mawili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya Caen. Ikumbukwe kuwa NEYMAR na CAVANI hawapo wana majeruhi kwahiyo Mbappe pamoja na Di Maria wamekuwa wakiongoza safu ya ushambuliaji na wamekuwa wakifanya vyema. PSG inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 huku timu ya pili, LILLE wakiwa na pointi 54. 


7. MARIO BALOTELLI HAACHI VITUKO:
Hayo ndio maneno unayoweza kusema kuhusu Mario Balotelli mara baada ya kufunga goli wikiendi hii na kushangilia kwa kuchukua simu na kupiga selfie na kuipost hapo hapo. Strange nhaa? Ila alistahili kwnai goli lilikuwa kali sana la mtindo wa Bicycle kick. Ni kama tiktaka fulani hivi. Baloteli kwa sasa yupo katika klabu ya MARSEILE kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu. 


8. NBA PAMOTO: 
Kwenye ligi pendwa ya mpira wa kikapu duniani NBA, zilichezwa mechi nyingi kutoka kanda zote za mashariki na magharibi na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: 
Cavaliers 93-129 Pistons, Pacers 112-117 Magic, Heat 117-88 Nets, Mavericks 81-111 Grizzlies, 76ers 117-120 Warriors, Spurs 116-102 Thunder, Jazz 115-111 Bucks, Nuggets 112-120 Pelicans, Suns 118-109 Lakers, Hornets 108-118 Trail Blazers, Clippers 128-107 Knicks, Celtics 104-115 Rockets, Bulls 118-123 Hawks.


9. MANCHESTER CITY .
Manchester City wamegoma kutoa tamko lolote kuhusu tuhuma mpya za kuvunja kanuni za FFP kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky sports. Jarida la Ujerumani Der Spiegel wameibua ujumbe wa barua pepe (emails) ambazo zimevuja ambazo zinaonesha mmiliki Sheikh Mansour aliweka fedha zake binafsi moja kwa moja kwenye klabu ili kuongezea juu yake fedha walizopata kutokana na wadhamini na kuiwezesha City kukidhi mahitaji ya FFP.


Kanuni za UEFA zimeweka kiwango cha fedha ambacho mmiliki anaruhusiwa kuingiza kwenye klabu na Mansour kupitia mfuko wake wa uwekezaji - Abu Dhabi United Group, anatuhumiwa kuzidi kiwango hiko. 

Kwa kujibu kuhusu email hizo ambazo zimevuja, City wamesema: "Hatutoa tamko lolote kuhusu nyaraka zozote ambazo zimearifiwa kudukuliwa au kuibiwa kutoka City Football Group na mfanyakazi wa City na mtu yoyote anayehusika na City. Jaribio la kutaka kuharibu heshima ya klabu inaonekana wazi". City tayari wanachunguzwa na UEFA kuhusu emails ambazo ziliwekwa hadharani na jarida la Der Spiegel mnamo mwaka jana kuhusu kuvunja kanuni za FFP.

Wakati huo huo, Der Spiegel waliwatuhumu City kwa kushindwa kutoa taarifa hadharani kuhusu mchezaji wao kwa kipindi hiko Bruno Zuculini kwamba alikiwa ana milikiwa na upande wa tatu kitu ambacho hakiruhusiwi chini ya kanuni cha FA. Msemaji wa FA amesema, "tulikuwa tunajua kuhusu tuhuma hizo na tunazifanyia kazi"

10. MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA LIGI ZOTE WIKIENDI:
Torino 3-0 Chievo, Atalanta 3-1 Fiorentina, Udinese 2-1 Bologna, SPAL 1-2 Sampdoria, Marseile 2-0 Saint-Ettiene, Nice 1-0 Strasbourg, Lille 1-0 Dijon, Valencia 2-0 Athletic Club, Real Sociedad 0-2 Atletico Madrid, Real Betis 1-2 Getafe, Villareal 1-2 Alaves, Watfors 2-1 Leicester, Westham 2-0 Newcastle, Manchester United 3-2 Southampton, Chelsea 2-1 Fulham, Mtibwa sugar 2-0 Mbao Fc, Singida 2-1 TZ Prisons, Mbeya City 0-0 Ndanda, Kagera sugar 2-0 Lipuli, Fc Augsburg 2-1 Dortmund, Borussia M'gladbach 1-5 Fc Bayern Munich, Fc Nurnberg 0-1 RB Leipzig, nk

Loading...

No comments: