SPORTS WEEKEND ROUND-UP: SIMBA YATAFUNA WAKONGO BILA HURUMA, YANGA CHALI KWA LIPULI, MAN CITY WAFANYA COMEBACK YA HATARI HUKU UNITED WAKITOLEWA FA, JUVENTUS WAPOTEZA MECHI KWA MARA YA KWANZA MSIMU HUU, LIVERPOOL NA MANE WAPO MOTO, ZIDANE AANZA NA USHINDI MADRID, GRIEZMANN AJUTIA KUTOKWENDA BARCA, BARCELONA MAMBO MBELE KWA MBELE... - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 18, 2019

SPORTS WEEKEND ROUND-UP: SIMBA YATAFUNA WAKONGO BILA HURUMA, YANGA CHALI KWA LIPULI, MAN CITY WAFANYA COMEBACK YA HATARI HUKU UNITED WAKITOLEWA FA, JUVENTUS WAPOTEZA MECHI KWA MARA YA KWANZA MSIMU HUU, LIVERPOOL NA MANE WAPO MOTO, ZIDANE AANZA NA USHINDI MADRID, GRIEZMANN AJUTIA KUTOKWENDA BARCA, BARCELONA MAMBO MBELE KWA MBELE...


1. SIMBA YATAFUNA WAKONGO BILA HURUMA TAIFA NA KUFUZU HATUA YA ROBO FAINALI: 
Klabu ya Simba Sports Club ya jijini Dar es salaam, juzi usiku iliwashangaza watanzania wengi kwa kuweza kuonyesha kabumbu bora kabisa na kushinda mchezo huo kwa magoli 2-1 dhidi ya klabu ya AS Vita ya nchini DRC Kongo. Mechi hiyo ya mwisho ya hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa barani Afrika ilikuwa ndio inayoamua nani afuzu na nani asifuzu katika kundi D ambalo liliundwa na timu kama Al-Ahly, JS Saoura, AS Vita pamoja na Simba SC. 

Goli la dakika ya 90 la kiungo Clautious Chama liliweza kuwafanya wekundu wa msimbazi kufuzu hatua ya robo fainali wakiungana na Al-Ahly kutoka kundi D ambao waliifunga JS Saoura. Hongera kwa Simba na kila la kheri katika hatua zinazofuata. 


2. YANGA CHALI KWA LIPULI: 
Mashabiki wa Yanga wana hali mbaya sana. Unajua kwanini? (1) Timu yao imefungwa (2) Simba kashinda na kafuzu robo fainali. Katika mechi yao na klabu ya LIPULI FC, Yanga alijikuta akichapwa goli moja tu (1-0), goli lililofungwa na beki Haruna Shamte mnamo dakika ya 20 ya mchezo kwa kupiga faulo nzuri iliyoingia moja kwa moja langoni mwa Yanga. 


3. MAN CITY WAFANYA COMEBACK YA HATARI FA CUP, HUKU UNITED WAKIFUNGISHWA VIRAGO NA WOLVES:
Siku ya jumamosi ilikuwa ni siku ambayo mechi za robo fainali ya kombe la Emirates FA Cup zilikuwa zikichezwa. Timu kubwa za jiji la Manchester (Man United na Man City) zote zilikuwa kibaruani. Man United alikuwa akipambana na Wolves, wakati Man City alikuwa akipambana na Swansea City. 

Mpaka Half Time, Man City walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 na kila mtu aliona kuwa City wangepoteza mechi hiyo. Lakini mambo yaligeuka kwani Bernado silva na Sergio Aguero walihakikisha Comeback inakamilika na kushinda 3-2 na kufuzu kucheza nusu fainali ya FA. 

Wakati City akipita, United wao waliambulia kichapo cha 2-1 kutoka kwa Wolves na hata goli la Man United lilifungwa dakika za lala salama (95' Marcus Rashford) na kutolewa nje rasmi. 


4. JUVENTUS WANAPOTEZA MCHEZO WA KWANZA KATIKA LIGI KUU NCHINI ITALIA: 
Juventus pamoja na PSG zimekuwa timu ambazo zimecheza michezo mingi katika ligi kuu za barani Ulaya bila kupoteza. Lakini hayo yameisha jana kwa Juventus kupoteza mchezo wao dhidi ya GENOA kwa 2-0. 

Juve ambao walikuwa Ugenini walicheza bila wachezaji wao muhimu waliopumzishwa baada ya kuwa na kibarua kigumu katikati mwa wiki katika ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid. 


5. MANE & LIVERPOOL ARE ON FIRE: 
Nikikwambia kuwa Sadio Mane amefikisha magoli 17 sasa ya ligi kuu ya Uingereza unaweza kuamini? Si rahisi kwani alipotea mwanzo wa msimu lakini sasa amerudi katika makali yake na anafanya vyema mno hasa katika kipindi hiki ambacho staa wao Mohamed Salah hayupo katika ubora wake. 

Mane alifunga goli la kwanza katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Fulham hapo jana na kuiwezesha timu yake kuongoza ligi kwa muda huku Man City wakiwa bado hawajacheza mchezo wao. Goli la ushindi la Liverpool lilifungwa kwa mkwaju wa penati na James Milner dakika ya 81. 


6. ZIDANE AANZA VIZURI KWA USHINDI MADRID: 
 Najua utakuwa unajua kuwa klabu ya Real Madrid iliamua kumrudisha kazini aliyewahi kuwa kocha wao Zinedine Zidane na wakamfukuza kazi Santiago Solari. Sasa habari njema ni kuwa kocha huyo ameanza vyema kazi mara baada ya timu yake kushinda nyumbani 2-0 dhidi ya timu ya Celta Vigo mapema jumamosi. 

Magoli ya Madrid yalifungwa na kiungo ISCO ambaye alikuwa hachezeshwi na kocha Solari pamoja na BALE aliyefunga goli la pili na kukamilisha ushindi huo. 7. GRIEZMANN AJUTIA KUIKATAA OFA YA KWENDA FC BARCELONA
Moja ya habari zilizotapakaa katika vyombo vikubwa na vidogo vya habari za kimichezo duniani ni habari ya Majuto ya mshambuliaji na staa wa klabu ya Atletico Madrid, Antonio Griezmann akijutia kutokubali ofa ya klabu ya Barcelona baada ya kuona mwenendo mbaya wa klabu yake. 

Atletico Madrid imetolewa katika Copa Del Rey, Ligi ya mabingwa Ulaya, na kufungwa juzi ugenini 2-0 dhidi ya Athletic Club kunawaondoa katika mbio za Ubingwa kwani wanakuwa wameachwa point 10 dhidi ya vinara FC Barcelona. 

Griezmann hajioni akishinda makombe makubwa na klabu yake na hicho ndicho kinachomfanya ajutie kutokuondoka mwanzoni mwa msimu alipokuwa akitakiwa na Barca. 


8. BARCELONA MAMBO MBELE KWA MBELE, MESSI WAMOTO BALAA. 
Klabu ya FC Barcelona imeendelea kupata matokeo mazuri katika ligi kuu nchini hispania na kuzidi kujichimbia kileleni mwa ligi hiyo ikiwa zimebaki mechi chache tu ligi imalizike. Hii ni baada ya kupata ushindi mwingine wa nguvu ugenini dhidi ya Real Betis wa 4-1 huku Lionel Messi akiwa chachu ya ushindi huo kwa kufunga magoli 3 (hattrick) huku jingine likifungwa na Suarez. 

Loading...

No comments: