Steve Nyerere atoa siri kubwa ya Wema - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 29, 2019

Steve Nyerere atoa siri kubwa ya Wema


Steve Nyerere atoa siri kubwa ya Wema

Msanii wa filamu na mchekeshaji maarufu nchini, Steve Nyerere, ambaye pia ni mtu wa karibu sana wa Wema Sepetu, ametoa siri kubwa ambayo wengi walikuwa wanatamani kujua kutoka kwa mwanadada huyo.


Steve amekuja na jibu la nani aliyezama kwenye mahusiano na Wema kwenye mahusiano kwa sasa, baada ya kuchangia maoni yake kwenye ukurasa wa Instagram wa mwanadada huyo akimsifia shemeji yake mpya, baada ya kumposti.

Picha zima lilianza baada ya Wema kuposti video ya mwanaume huyo anayejulikana kwa jina la Danzak, ambapo Steve alikuja na kuandika ujumbe akisema, "shemeji katutendea haki kwa hii ngoma, daah katoa voko ya ajabu sana hakuna mtu anaimba kama uyu toka tumepata uhuru, huyu ni kiboko, nyimbo inayofuata imba naye”.

Ujumbe huu wa Steve Nyerere ni utambulisho tosha kuwa Wema Sepetu sasa anamilikiwa na msanii huyo, ambaye pia ana makazi yake nchini Oman huku akiwa na kazi nyingine yenye mkwanja mrefu ya urubani.

Kwa muda mrefu mlimbwende huyo amekuwa akificha maisha yake ya mahusiano, tangu alipokumbwa na skendo ya kuvuja video zake akiwa faragha na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la PCK mwishoni mwa mwaka uliopita.
Loading...

No comments: