SWR: ARSENAL YAINYAMAZISHA UNITED, CITY NA LIVER WAENDELEA KUFUKUZANA, SIMBA YACHAPWA ALGERIA, KMC WAWAPA YANGA POINTI 3 DAR, BARCA HAISHIKIKI LALIGA, BAYERN WAPINDUA MEZA RASMI, PIATEK AMFIKIA CR7 KWA MAGOLI ITALIA, MBIO ZA KUFUZU PLAYOFFS ZA NBA ZAENDELEA... - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 11, 2019

SWR: ARSENAL YAINYAMAZISHA UNITED, CITY NA LIVER WAENDELEA KUFUKUZANA, SIMBA YACHAPWA ALGERIA, KMC WAWAPA YANGA POINTI 3 DAR, BARCA HAISHIKIKI LALIGA, BAYERN WAPINDUA MEZA RASMI, PIATEK AMFIKIA CR7 KWA MAGOLI ITALIA, MBIO ZA KUFUZU PLAYOFFS ZA NBA ZAENDELEA...1. ARSENAL YAINYAMAZISHA MAN UNITED: Moja ya mechi ambayo ilikuwa ikisubiriwa na ikafuatiliwa sana wiki hii ni mechi ya ARSENAL Vs MANCHESTER UNITED iliyopigwa pale uwanja wa Emirates jijini London. Matokeo ya mechi hiyo yalikuwa ni 2-0 na yaliwafanya Manchester United kupoteza kwa Mara ya kwanza mechi ya ligi kuu chini ya Kocha wao mpya OLE GUNNAR SOLSKJAER. 


Alikuwa ni kiungo Granit Xhaka aliyeanza kuipatia Arsenal goli la kwanza mapema tu Dakika ya 16, goli lililochangamsha mchezo. Mpaka mapumziko ilikuwa ni 1-0. Kipindi cha pili kila timu ilitafuta nafasi ya kufunga lakini alikuwa ni Piere Emerick Aubeyang ambaye alikuja kufunga goli la pili la Arsenal kwa mkwaju wa penati huku akimuuza golikipa David De gea ambaye kwa Jana hakuonekana kuwa katika ubora wake uliozoeleka. Matokeo haul yanaifanya Arsenal ipande hadi nafasi ya 4 huku Man United ilishuka hadi nafasi ya 5. Chelsea wakiwa nafasi ya 6. 

2. MBIO ZA UBINGWA EPL, CITY NA LIVER BADO WANAFUKUZANA.
Wanakwambia "its not over till it's over" na hichi ndicho tunachokiona katika ligi kuu nchini England. Mafahari wawili (Liverpool Fc na Manchester City) Vado wanaendelea kufukuzana katika mbio za kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza huku kila timu ikiwa na nafasi ya kuubeba ubingwa huo. 


Alikuwa ni Raheem Sterling ambaye alikuwa SHUJAA wa mechi ya Man city dhidi ya Watford Baada ya kufunga Hattrick (magoli 3) kipindi cha pili na kuifanya Man City kuendelea kukaa kileleni mwa ligi. Mechi iliisha kwa matokeo Man City 3-0 Watford.

Sadio Mane pamoja na Roberto Firmino walifunga magoli mawili kila mmoja na kuhakikisha Liverpool wanashinda 4-2 dhidi ya Burnley na kujiweka vizuri kiendelea kutoa changamoto kwa mabingwa watetezi Man City. 

3. SIMBA WAKUBALI KICHAPO ALGERIA, SAOURA WALIPIZA KISASI. 
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara, Simba Sports Club ambao pia ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, wamejikuta wakichapwa ugenini nchini Algeria magoli 2-0 na timu ya JS SAOURA ya hukohuko.  


Ikumbukwe kuwa katika mechi ya kwanza iliyokutanisha mechi hizo katika uwanja wa taifa Dar es salaam Simba alishinda kwa mabao matatu. Kwahiyo ushindi wa JS SAOURA ni kulipiza kisasi ya kile walichofanyiwa na wekundu wa msimbazi hao. Simba NI LAZIMA WASHINDE MECHI YAO YA MWISHO dhidi ya AS VITA itakayofanyika hapa Dar es salaam ili waweze kupita kwenda hatua ya mtoano. 

4. KMC YAWAPA YANGA POINTI 3 TAIFA:
Klabu ya yanga jana ilipata ushindi wa 2-1 dhidi ya timu ya manispaa ya kinondoni maarufu kama KMC Fc. Katika mechi hiyo ambayo kila timu ilikuwa inahitaji pointi 3 muhimu, KMC walijikuta wakiwasaidia Yanga mara baada ya beki wa ALLY ALLY kujifunga dakika za lala salama na kuwapa Yanga goli la pili na la ushindi. Yanga bado wanaongoza ligi. 


5. BARCA HAISHIKIKI LALIGA, MADRID WAAMKA:
Fc Barcelona imeendelea kufanya vyema kwenye ligi kuu ya nchini hispania baada ya jumamosi kuibuka na ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya Rayo Valecano ambao walionekana wakali sana kipindi cha kwanza. Rayo walifunga mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Raul De Thomas lakini kabla ya mapumziko beki Gerald Pique alisawazisha kwa kuunganisha faulo iliyopigwa na Lionel Messi. 


Messi alikuja kuifungia Barca goli la pili kwa Penati, na Luis Suarez akafunga goli la 3 kutokana na pasi ya Ivan Rakitic ambaye ndio alikuwa katoka kuingia muda si mrefu. Bado Barcelona wanaongoza ligi. 

Wapinzani wao wakubwa, REAL MADRID na wao wakaamka kutoka usingizini kwa kushinda 4-1 dhidi ya Real Valladolid hapo jana huku Kareem Benzema akitupia goli 2. Huu ni ushindi wa kwanza kwa madrid baada ya kuwa na matokeo mabaya hivi karibuni hasa dhidi ya wapinznai wao wakubwa FC BARCELONA. 

6. RASMI SASA FC BAYERN WAMEPINDUA MEZA, WAPO KILELENI. 
Umeshawahi kusikia msemo wa "kama unajua, unajua tu?" basi huo msemo unaendana sana na kinachotokea sasa katika ligi kuu ya ujerumani maarufu kama Bundesliga. Baada ya kuachwa kwa muda mrefu na Borussia Dortmund ambao walianza vyema sana msimu huu, Bayern wamerudi katika kiwango chao kizuri na sasa wamewafikia Dortmund na kuwaacha kwa tofauti ya magoli. 


Hakuna aliyekuwa akiipa Bayern nafasi ya kuchukua kombe la msimu huu hasa ikizingatiwa walikuwa wameachwa takribani pointi 16 na Borussia kipindi fulani. Lakini ukomavu wa mabingwa hao mfululizo wa Bundesliga kwamiaka 6 mfululizo umeonekana na hatuoni nafasi ya Dortmund tena katika kutoa changamoto kwa Bayern. Wamefeli sana. 

7. PHILLIPE COUTINHO AHUSISHWA NA MAN UNITED:
Kiungo na winga wa klabu ya FC BARCELONA ambaye bado mambo hayamwendei sawa, Philipe Coutinho ameanza kuhusishwa na kurudi katika ligi kuu ya Uingereza lakini sio kwenye timu aliyokuwepo kabla ya LIVERPOOL bali MANCHESTER UNITED. Inasemekana Manchester wapo tayari kutoa dau nono la Pauni Milioni 100 kumpata Coutinho katika dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi. 


8. PIATEK AMFIKIA RONALDO KWA MAGOLI SERIE A:
Mshambuliaji mpya wa klabu ya AC MILAN Krzysztof Piatek ameendelea kuonyesha kiwango bora kabisa msimu huu mara baada ya kuendelea kuzifumania nyavu na sasa amefikisha magoli 19 katika ligi hiyo ya SERIE A huku akilingana na mkali wa kufunga wa JUVENTUS, Cristiano Ronaldo. Wote wana magoli 19 kwa sasa. Nani atamaliza juu ya mwezake? hilo swali nakuachia wewe msomaji wangu.

Piateka alifunga goli la pili katika ushindi wa 2-1 wa Milan dhidi ya Chievo Verona.9. NBA: LAKERS WAZIDI KUCHAPWA, JUHUDI ZA LEBRON HAZITOSHI KUWAOKOA:
Katika ligi kuu ya kikapu nchini Marekani maarufu kama NBA, michezo mingi ilichezwa wikiendi hii na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo: HAWKS 112-114 NETS, TIMBERWOLVES 135-130 WIZARDS, LAKERS 107-120 CELTICS, BUCKS 131-114 HORNETS, TRAIL BLAZERS 127-120 SUNS, PISTONS 131-108 BULLS, 76ERS 106-89 PACERS, HEAT 104-125 RAPTORS.10. MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI KATIKA LIGI MBALIMBALI DUNIANI:
Newcastle 3-2 Everton, Cardiff 2-0 Westham, Chesea 1-1 Wolves, Southampton 2-1 Spurs, Leicester 3-1 Fulham, Huddlesfield 0-2 Bournermouth, Crystal palace 1-2 Brighton, Monac0 1-1 Bordeaux, Dijon 1-1 Reims, Amiens 2-1 Nimes, Strasbourg 2-2 Lyon, Fiorentina 1-1 Lazio, Sassuolo1-1 Napoli, Sampdoria 1-2 Atalanta, Intermillan 2-0 SPAL, Frosinone 1-2 Torino, Bologna 2-0 Cagliari, Levante 0-2 Villareal, Girona 2-3 Valencia, Sevilla 5-2 Real Sociedad, FC Bayern 6-0 Wolfsburg, Werder Bremen 4-2 Schalke 04, Dortmund 3-1 Stuttgart, RB Leipzig 0-0 Augusburg, Hannover96 2-3 Bayern Leverkusen,


Loading...

No comments: