TAIFA STARS KUCHUANA NA UGANDA “THE CRANES” KATIKA MCHEZO WA KUWANIA KUFUZU KUCHEZA MICHUANO YA AFCON 2019 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 8, 2019

TAIFA STARS KUCHUANA NA UGANDA “THE CRANES” KATIKA MCHEZO WA KUWANIA KUFUZU KUCHEZA MICHUANO YA AFCON 2019

Kocha Mkuu wa Timu ya Soccer ya Tanzania “Taifa Stars” Emmanuel Amunike akizungmza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akijtajai kikosi kitakachochecha mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 dhidi ya timu ya Uganda “The cranes” mnamo Machi 24 mwaka huu.

Timu ya Soka ya Tanzania “Taifa Stars” inatarajia kucheza mchezo wake wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 dhidi ya timu ya Uganda “The cranes” mnamo Machi 24 mwaka huu. 

Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mnamo Machi 24, saa 12 jioni na endapo itafanikiwa kushinda mchezo huo, Taifa Stars itakuwa imejikatia tiketi ya kushiriki AFCON nchini Misri baadaye mwaka huu. 

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema ana matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo dhidi ya wapinzani wake kutoka Uganda. 

“Timu yetu imejiandaa vya kutosha kuhakikisha inashinda mchezo huu,” alisema Amunike wakati wa mkutano na waandishi wa habari huku akiwataka watanzania kuiunga mkono timu hiyo ya Taifa siku ya mtanange huo. 

Kapteni wa Taifa Stars na mchezaji wa klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta ataongoza kikosi hicho. 

Kwa upande wake, Afisa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), George Mango amesema kampuni hiyo imekuwa ikihakikisha inakiwezesha kikosi hicho kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mtanange huo na hatimaye iweze kuibuka na ushindi kuelekea AFCON nchini Misri. 

“Siku zote kinywaji cha Serengeti Premium Lager ni shabiki mkuu wa Taifa Stars na mdhamini mkuu pia. Katika mchezo huu tumejidhatiti kuhakikisha timu yetu inaibuka na ushindi ambao ni utakuwa fahari kwa Taifa letu na kwa kinywaji chetu cha Serengeti,” alisema Mango. 

Mango aliwataka mashabiki wa soka nchini kufika kwa wingi siku ya mchuano huo ili kuwapa hamasa wachezaji kwaajili ya kuipa ushindi timu hiyo ya Taifa.

Loading...

No comments: