Tambua Chanzo cha Kwikwi na Tiba ya Haraka! - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 12, 2019

Tambua Chanzo cha Kwikwi na Tiba ya Haraka!

Kwikwi (Chechevu) ni mkazo wa ghafla na usio wa hiari wa msuli wa kiwambo unaosababisha pumzi kutokea kinywani na sauti ya kugugumia kutokana na hewa kuingia kwenye umio. Vitu vinavyochangia kwikwi ni pamoja na kunywa pombe, soda yenye gesi, maji ya moto, kutafuna bigijii/chingamu (chewing gum), kula vyakula vyenye viungo, kula haraka sana au kula au kunywa chochote kilicho baridi sana baada ya kula cha moto.


Kuwa na mkazo (stress), hisia kali kama furaha (kucheka sana), tabia kama kula sana, kula haraka sana, kunywa vinywaji vinavyofanya tumbo kujaa gesi kama soda huchangia mtu kupata kwikwi.Watoto wanakula au kunyonya mara nyingi zaidi ya watu wazima hivyo kuruhusu hewa nyingi zaidi kuingia kinywani kitu kinachopelekea watoto kupata sana kwikwi.Ingawa kwikwi nyingi huisha zenyewe tu baada ya muda mchache ila unaweza kuvuta pumzi nzito na kisha kubana hewa kwa muda mrefu ikiwa kwikwi inasababishwa na uwepo wa hewa nyingi tumboni itafanya kwikwi kuisha.


Vuta magoti yako usawa wa kifua na inamia mbele, kunywa maji ya baridi sana, tafuna sukari, tafuna limao au lamba siki (vinegar).


Wataalamu wanadai kukanda shingo pale ilipo neva ya freniki inayochochea daframu husaidia kutuliza kwikwi. Ikiwa umejaribu njia hizi rahisi na kwikwi inaendelea kwa muda mrefu (zaaidi ya masaa 48 au inarudia mara kwa mara) ni vyema kutafita msaada wa kitabibu.
Loading...

No comments: