TANZANIA MBIONI KUISHIWA DAWA ZA KUTULIZA MAUMIVU MAKALI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

TANZANIA MBIONI KUISHIWA DAWA ZA KUTULIZA MAUMIVU MAKALI


Taarifa hii ni kwa mujibu wa tovuti ya 'The East African' imeelezwa kuwa taasisi ya Wagonjwa wa Saratani ya Ocean Road ilitoa taarifa za tishio la kuisha kwa dawa hizo tangu mwaka 2018. 

Mmoja wa maafisa wa taasisi hiyo ameeleza kuwa kiasi cha dawa hizo kilichosalia hakiwezi kudumu kwa muda wa mwezi mmoja. 

Aidha, Afisa wa Bohari ya Dawa (MSD), Mwanashehe Juma, amethibitisha kuwa idara yao ilipokea ombi la dawa hizo kutoka Taasisi ya Ocean Road. 

Amesema mchakato wa ununuzi wa ugavi wa dawa hizo ndio umechelewesha kupatikana kwa dawa hizo kwa wakati. 

Hata hivyo amethibitisha kuwa dawa hizo zitaanza kupatikana kuanzia mwezi ujao. 

Loading...

No comments: