TANZANIA NA RANKING ZA CAF KATIKA KUPATA NAFASI ZAIDI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 18, 2019

TANZANIA NA RANKING ZA CAF KATIKA KUPATA NAFASI ZAIDI


Hapo nyuma niliandika kwa kirefu kidogo maana na jinsi zinavyofanya kazi hizi RANKING za CAF katika kupata nafasi za nyongeza katika nchi uwakilishi.

TANZANIA: 
Tanzania kama mwanachama wa CAF juzi baada ya Simba kushinda imepanda RANKING na kufikisha point 18 na kuwa kwenye nafasi ya 12 toka ya 17 ilipokuwa kabla ya mechi hii na kufanya au kuweka matumaini ya kuongezeka Timu kuwa hai zaidi. 

WASHINDANI WENZETU: 
Katika kutafuta nafasi Mbili zilizokuwa Wazi ili ziwezekutimia nafasi 12 za nchi kuna nchi 4 zinagombea nafasi hiyo nazo ni Angola, Tanzania, Congo Brazavile na Ivory Coast. 

Baada ya mechi za CAF Champion League Simba kwa Tanzania imesonga mbele huku Asec Mimosas ya Ivory Coast ikitolewa na kubaki na point 15 hivyo kutokuwa mshindani wetu tena. 

Kwenye CAF Confederation Cup kuna Petro Luanda ya Angola ambao itacheza na Gor Mahia pia Otoho ya Congo Brazavile inacheza na Raja Casablanca hawa wawili ndio wapinzanu wetu wakuu. 

ANGOLA:
Petro Luanda inaifanya Angola mpaka sasa iwe na point 19 kusubiri mechi na Gor Mahia ikishinda inakuwa na point 29 nakwenda Quarter final, ikifungwa inakuwa -- 3rd ina point 24 ikiwa ya 4th inakuwa na point 21.5

CONGO BRAZAVILE:
Otoho ya Congo ina point 9 baada ya matokeo ikishinda inakuwa Quarter final na point 19 ila ikifungwa inakuwa na point 14.

JICHO LETU:
Ili Tanzania iweze kupata nafasi za ziada kwenye mashindano ya 2020/2021 kutokana na fact hizo hapojuu lazima haya yahusike:
1. Otoho afungwe ili aondoke kwenye nafasi nasi tutabaki na Angola hivyo Direct tumekamata nafasi za ziada.
2. Petro Luanda ya Angola afungwe ili abaki na point zake 21.5 tukazitafute za ziada kwenye semi final.
3. Otoho akishinda kwenda Quarter final imebidi tusubiri mpaka tuvuke semi final. 
Loading...

No comments: