TEGEMEA KUMWONA MOURINHO NDANI YA REAL MADRID MUDA SI MREFU - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 6, 2019

TEGEMEA KUMWONA MOURINHO NDANI YA REAL MADRID MUDA SI MREFU


Jose Mourinho ndio chaguo la kwanza kuinoa Real Madrid na tayari klabu imeshafanya mawasiliano naye, kwa mujibu wa Rais wa zamani wa klabu hiyo Ramon Calderon.

Kocha wa sasa wa Real Madrid , Santiago Solari yupo kwenye presha kubwa baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo dhidi ya Barcelona na kutolewa kwenye mashindano ya UEFA dhidi ya Ajax jana usiku. 

Mourinho ambaye aliondoka Real mwaka 2013, wiki iliyopita alisema kwamba amefurahishwa kuhusishwa na kurejea Bernabeu na ameonekana kuwa chaguo mashuhuri la mashabiki ambao walikuwa wakiimba jina lake baada ya mechi dhidi ya Ajax kuisha.

Rais wa Mdrid Florentino Perez anahitaji "kuangusha bomu" ili kuwatuliza mashabiki na anatarajiwa kumuita Mourinho, kocha pekee ambaye anamuheshimu" kwa mujibu wa Calderon.

Calderon ameiambia Sky Sports, "Sina shaka hata kidogo kwamba Mourinho ndio chaguo la kwanza la Rais . Alipigiwa simu wiki iliyopita."

"Mara ya kwanza ilikuwa siku ambayo Zinedine Zidane aliondoka klabuni , Mourinho alikuwa Manchester United na alisema sio muda sahihi wa kurudi , labda sasa hivi yupo huru inawezekana. Nafikiri kuna nafasi kubwa sana atakuwa kwenye benchi msimu ujao."
Loading...

No comments: