TETESI: ALLEGRI KUIKACHA JUVE MWISHO WA MSIMU, CONTE KUREJEA JUVENTUS. - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 4, 2019

TETESI: ALLEGRI KUIKACHA JUVE MWISHO WA MSIMU, CONTE KUREJEA JUVENTUS.


Moja kati ya tetesi inayozagaa sana kwa sasa ni hii ya kuwa klabu ya Juventus yenye maskani yake jijini Turin, wameandaa mpango wa kumrejesha kocha wao zamani Antonio Conte klabuni kwa mujibu wa taarifa kutoka Corriere Dello Sport. 

Tetesi zimeanza kuibuka kwamba kocha wao wa sasa Massimiliano Allegri huenda akaondoka Turin mwishoni mwa msimu huu. 

Nyuma ya pazia, vinara hao wa Serie A wameanza kuandaa mazingira ya kumrejesha Conte huku kocha huyo wa zamani wa Chelsea ameonesha nia ya kutaka kurejea Bianconeri. 

Unadhani ni wakati sahihi wa Conte kwenda Juve na Allegri kuondoka?

Loading...

No comments: