TETESI ZA USAJILI: ARSENAL WAPO TAYARI KWA SAMUEL UMTITI - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

TETESI ZA USAJILI: ARSENAL WAPO TAYARI KWA SAMUEL UMTITI


Taarifa za kuaminika zinasema kuwa klabu ya Arsenal wapo tayari kumsajili beki wa kati FC Barcelona Samuel Umtiti endapo klabu yake itamuweka sokoni hivi karibuni. 

Raul Sanllehi, ambaye kwasasa anashikilia nafasi ya Mkurugenzi wa Michezo kwa muda katika klabu ya Arsenal mpaka atakapopatikana mpya ndiye ambaye alihusika kwa kiasi kikubwa kumpeleka Umtiti Nou Camp kutokea klabu ya Lyon. 

Umtiti amekuwa akiandamwa na majeruhi ya hapa na pale jambo linalomfanya asipate wakati mzuri wa kuitumikia klabu ya Barcelona na kwa sasa klabu hiyo ya Hispania wapo mbioni kumsajili beki mholanzi kinda Matt Deligt na inabidi Umtiti auzwe. 
Loading...

No comments: