TETESI ZA USAJILI: MALCOM KWENYE RADA ZA INTERMILLAN - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

TETESI ZA USAJILI: MALCOM KWENYE RADA ZA INTERMILLAN


Winga wa klabu ya FC Barcelona mbrazil Malcom, anahitajika na klabu ya Serie A Inter Milan majira ya kiangazi kwa mujibu wa taarifa kutoka Calcio Mercato. 

Inter Milan walikuwa tayari kumsajili Malcom mwezi Januari mwaka huu kwa mkopo lakini Barcelona waligoma kufanya biashara ya miezi sita wakisisitiza kwamba wanataka dili la uhamisho wa kudumu ili warudishe angalau kiasi cha fedha walicholipa kumsajili cha Euro Milioni 40. 

Malcom amekuwa akikosa nafasi katika kikosi cha kocha Ernesto Valverde na hatma yake imekuwa katika mashaka kwa muda mrefu sasa. 

Loading...

No comments: