TETESI ZA USAJILI: PERISIC KUTIMIZA NDOTO ZA KUTUA JIJINI LONDON? - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

TETESI ZA USAJILI: PERISIC KUTIMIZA NDOTO ZA KUTUA JIJINI LONDON?


Klabu ya Tottenham Hotspurs wamefungua mazungumzo na klabu ya Inter Milan ya Italia kuhusu uwezekano wa kupata saini ya winga wa kushoto Ivan Perisic majira ya kiangazi kwa mujibu wa taarifa kutoka TuttoMercartoWeb. 

Winga huyo wa kimataifa wa Croatia ameripotiwa anaweza kupatikana kwa dau la Pauni Milioni 30. 

Ikumbukwe kuwa mnamo dirisha la usajili la kiangazi kabla ya msimu huu kuanza, Perisic alikuwa akihitajika mno na klabu ya Arsenal ambayo nayo ni ya jiji la London lakini InterMillan hawakuwa tayari kumuuza. 

Je Perisic atafanikiwa kuondoka Italia?
Loading...

No comments: