TFDA: "WALAJI WA DONA HATARINI KUUGUA SARATANI YA INI" - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 16, 2019

TFDA: "WALAJI WA DONA HATARINI KUUGUA SARATANI YA INI"


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema ulaji wa vyakula vilivyochafuliwa na kiasi kikubwa cha sumukuvu husababisha madhara ya kiafya ya muda mfupi na muda mrefu

Madhara ambayo mtu anaweza kuyagundua baada ya muda mrefu kupita ni ya kuugua saratani ya ini na madhara ya muda mfupi ni mlaji kuugua ugonjwa wa kuhara.

Sumu hiyo hupatikana kwenye mazao ya nafaka hasa mahindi na karanga, na kwamba walaji wa ugali wa dona wapo hatarini zaidi ikiwa hatua za uandaaji wa chakula hicho hautazingatiwa

Hayo yamesemwa na Msemaji wa TFDA, Gaudensia Simwaza alipoulizwa kuhusu hatua zinazochukuliwa kudhibiti waandaaji wa unga wa dona nchini na madhara yanayoweza kumpata mtu endapo atakula chakula hasa ugali wa dona ambayo imechafuliwa na sumukuvu

Dona ina lishe na ni sahihi kuliwa, shida ni maandalizi ya unga wa dona. Ni lazima anayeandaa aoshe kwa umakini na usahihi kwani wengi huhifadhi mahindi na dawa.
Loading...

No comments: