TFF YAFUNGUKIA JEZI ZA ‘MSALABA’ - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Sunday, March 24, 2019

TFF YAFUNGUKIA JEZI ZA ‘MSALABA’

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekana kuhusika na jezi za timu ya taifa 'Taifa Stars' zenye alama ya msalaba zinazosambaa mtandaoni.


Kwa mujibu wa taarifa iliytolewa na Afisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo kwa vyombo vya Habari, TFF imesema haizitambui na haihusiki na jezi hizo, na kutoa onyo kali kwa wauzaji wa jezi hizo.

“TFF haihusiki na jezi hiyo ambayo si sehemu ya jezi inayotumiwa na Timu ya Taifa, tunawaonya wote wanaoza jezi ambazo si sahihi, kuacha mara moja kabla TFF haijachukua hatua kali”, imeeleza taarifa hiyo

Jezi hizo (pichani hapo juu) zenye alama ya msalaba kwa mbele huku kikiwa na nembo ya TFF zilizua gumzo mtandandoni na wengi kuoneshwa kukuchukizwa na jezi hizo.


 Isome hapa taarifa hiyo


Waziri Mkuu Atembelea Kambi Ya Stars .......Kamati Yaahidi Milioni 10 Kwa Kila Mchezaji, Iwapo Watavuka

Loading...

No comments: