TONY GALE: "SERA MBOVU YA UPANGAJI WA KIKOSI CHA FULHAM IMEMHARIBIA KAZI RANIERI" - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 1, 2019

TONY GALE: "SERA MBOVU YA UPANGAJI WA KIKOSI CHA FULHAM IMEMHARIBIA KAZI RANIERI"

Ranieri

Ikiwa ni masaa machache yamepita tangu kutangazwa kwa uamuzi wa labu ya Fulham kumfungia virago kocha wao Claudio Ranieri, aliyewahi kuwa beki wa klabu ya Fulham, Tony Gale, amefunguka na kusema kuwa sera mbovu ya upangaji wa kikosi chake pamoja na mbinu zisizo sahihi zimechangia sana kocha huyo kufukuzwa kazi hapo jana mchana. 

Ranieri ambaye amefukuzwa siku ya alhamisi mchana, amekaa klabuni hapo kwa jumla ya miezi minne tu na amehusika katika mechi 17 tu katika michuano yote timu hiyo inayoshiriki.  

Muitaliano huyo alifukuzwa kazi mara tu baada ya Fulham kufungwa 2-0 na Southampton siku ya jumatano ambapo pia mashabiki walisikika wakipaza sauti zao wakisema "Haujui unachokifanya" pale Ranieri alipokuwa anafanya mabadiliko ya wachezaji katika kipindi cha pili cha mchezo. 

Gale anaamini kuwa kushindwa kwa Ranieri ni swala la kimbinu na kiufundi zaidi. "Sishangazwi sana na kufukuzwa kwake kwani nilikuwepo Southampton jumatano uwanjani na wote tulishuhudia mfumo wa ajabu aliouweka na kuwafanya wachezaji wake bora washindwe kufanya majukumu yao ipasavyo" Alisema Gale aliyewahi kuichezea Fulham kwa miaka 7 kuanzia mwaka 1977. 

"Alikuwa hawachezeshi wachezaji wake wazuri kama Ryan Sessegnon pamoja na Tom Cairney ambao ni lazima na muhimu waanze kwenye kila mechi. Nilikuwa sielewi kabisa tunachokifanya kwa hizi wiki 4 hadi 5 zilizopita kwa kweli na ndio maana sijashangazwa na hizi taarifa za yeye kufukuzwa." aliendelea Gale. 

"Walikuwa wapo vyema sana msimu uliopita, jambo la muhimu angeimarisha eneo la ulinzi kwanza kwani wamekuwa wakiruhusu magoli zaidi ya 2 karibia kila mechi. Yeye aliwaza kufunga zaidi kuliko kuweka ulinzi madhubuti." Alimalizia Gale. 


Loading...

No comments: