TOTTENHAM WAPEWA ONYO KUHUSU HARRY KANE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Monday, March 11, 2019

TOTTENHAM WAPEWA ONYO KUHUSU HARRY KANE


Klabu ya Tottenham Hotspurs watalazimika kutwaa mataji ili waweze kumshawishi Harry Kane kuendelea kubaki klabuni hapo amesema mshambuliaji wa zamani wa Spurs, Teddy Sheringham. 

Sheringham hakutwaa taji lolote katika kipindi cha miaka saba ndani ya Spurs katika vipindi viwili tofauti.

Hata hivyo katika kipindi cha miaka minne ndani ya Man United (alitoka Spurs akahamia Manchester United na baadaye kurejea Spurs) alitwaa mataji matatu ya EPL, moja la UEFA na moja la FA. 

"Harry atakuwa anatamani kutwaa mataji. Atakuwa anataka kucheza katika daraja la juu sana. Kuhamia Uwanja mpya kunaweza kumbakiza Harry lakini bado atakuwa anataka kutwaa mataji."

"Sasa hivi wanakaribia kufikia juu lakini kwa Harry hiyo haitoshi kwasababu yeye mwenyewe kafika juu." alimalizia Sheringham. 
Loading...

No comments: