TRIPPLE K THEORY-KUSAMEHEANA,KUELEWANA,KUSIKILIZANA NDO MPANGO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Friday, March 15, 2019

TRIPPLE K THEORY-KUSAMEHEANA,KUELEWANA,KUSIKILIZANA NDO MPANGO


Kiburi hakitakusaidia kwenye Mapenzi,Ni sawa na kupika wali unaonukia halafu unanyunyizia Sumu ya Panya madai yajo uongezee ladha,unajiua mwenyewe tu.

 Kununa hakukusaidii kujenga penzi,sanasana unajiongezea nundu tu usoni,kuna watu ukiwanunia wala hawana muda,wanakukaushia kama Kinyago,unajiumiza mwenyewe.Penzi linapaswa kuleta raha,na pale kwenye karaha mnatatua fasta mrudi kwenye raha

 Dawa ya penzi bora ni Kusikilizana,Kuelewana,na Kusameheana(Tripple K)...Kama mmeamua kusafiri kwenye Boti moja ya Mahaba saidianeni kuiendesha boti mfike salama,sio nahodha anaendesha halafu wewe uko bize kutoboa mtumbwi na misumari,hamtafika mtazama tu.

Na misumari yenyewe ni kununanuna bila sababu,maringo,ubishi,kiburi na kujiona ww uko juu kuliko mwenzio.Mapenzi ni matamu ukiyaelewa na ni machungu kwa woteeee mlio bize na misumari.

Jiangalie upya,kama una misumari tafadhali itupe,kamsaidie nahodha kuendesha boti yenu
Loading...

No comments: