Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yatangaza Kuongeza Vituo Vya Kupigia Kura 2020 - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 6, 2019

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yatangaza Kuongeza Vituo Vya Kupigia Kura 2020


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imeongeza vituo vya kupigia kura 858 kutoka 36,549 vya mwaka 2015  ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage  ameyasema hayo leo Jumanne Machi 5,2019 alipokuwa akizungumza na wawakilishi wa vyama vya siasa.

Mbali na kuongeza idadi ya vituo, Jaji Kaijage amesema vituo 6,208 vimebadilishwa majina na vituo 817 vimehamishwa kutoka kijiji/mtaa mmoja kwenda mwingine.

Kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura, Jaji Kaijage amesema mchakato wa kupata vifaa vya kukarabati machine za BVR umekamilika. 
Loading...

No comments: