TUNDU LISSU ATOA SIKU 14 KULIPWA MSHAHARA WAKE - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 28, 2019

TUNDU LISSU ATOA SIKU 14 KULIPWA MSHAHARA WAKE

Akizungumzia barua yake kwa uongozi wa Bunge, amesema aliwaagiza mawakili wake kuwasiliana na uongozi wa Bunge ili kufahamu ni lini wataanza kumpatia tena mshahara wake na stahiki za kibunge.


“Mawakili wangu wamemwandikia barua Katibu wa Bunge, Kagaigai ya kumtaka kulipa mshahara na posho zangu za kibunge za tangu Januari mwaka huu. pia walimpa siku 14 kutekeleza madai, vinginevyo tutafungua madai Mahakama Kuu”, amesema Lissu.

Machi 14, 2019 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu aliibua madai ya kutoingizwa na mshahara wake na Mhimili wa Bunge madai ambayo Spika wa Bunge, Job Ndugai alijibu kuwa alipaswa kuuliza uongozi wa Bunge juu ya mshahara wake.

Akizungumzia swala hilo, Spika Ndugai alisema, "kiukweli sijasikia lolote lakini hayo madai ya mshahara alimwandikia Spika barua kwamba hakupata mshahara wake na akajibiwa ni kwanini hakupewa mshahara wake?".


Chanzo:EATV.TV
Loading...

No comments: