UBER WAZINDUA APP YA UBER LITE ;Ndogo, Rahisi na Hakika - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Tuesday, March 19, 2019

UBER WAZINDUA APP YA UBER LITE ;Ndogo, Rahisi na Hakika


Uber Lite ni app mpya ambayo haitumii nafasi kubwa ya simu yako na inaweza kufanya kazi kwenye simu yoyote ya Android wakati mtandao si mzuri

Dar es Salaam, Machi 19, 2019 - Leo kampuni ya Uber imezindua app ya Uber Lite: app mpya, nyepesi na njia rahisi ya kupata huduma za Uber. Uber Lite ni toleo jipya la App ya Uber lililorahishwa na linaweza kutumika kwenye simu yoyote ya Android na halichukui nafasi kubwa ya simu pamoja na kwamba toleo hili halitumii bando kubwa. Pia utaratibu wa kujifunza na kuitumia umerahisishwa, na imejengewa uwezo wa kufanya kazi hata katika maeneo ambayo hayana mtandao mzuri.

Alon Lits, Meneja wa Uber Kusini mwa Jangwa la Sahara anaelezea, "Kila siku maelfu ya Watanzania wanategemea mfumo wa Uber kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine sambamba na kufanya shughuli za kuwaingizia kipato, tunafahamu kwamba toleo moja la Uber haliwezi kukidhi tofauti za kimtandao, aina za simu na mahitaji ya wasafiri kote nchini. Baada ya kufanya utafiti wa kina, tumeunda hii app mpya kwa kuzingatia maoni ya wasafiri lengo likiwa ni kuwarahisishia utaratibu wa kutumia mfumo huu na matokeo yake ni kuzinduliwa kwa Uber Lite."

Uber Lite imeundwa ili iharakishe na kurahisisha utaratibu wa kuita gari sambamba na kutumia bando kidogo kwenye maeneo ya muunganisho wa (2G), kwenye simu za Android, na kwa wateja wanaotumia bando ndogo.

Zifuatazo ni faida za toleo hili:

Haichukui nafasi kubwa ya simu : Ukubwa wa Uber Lite ni chini ya 5MB ukiipakua (hiyo ni sawa na selfi 3 tu). Faida ya kuwa na app ndogo ni kwamba inaacha nafasi kubwa ya kutunza selfi na app nyingine. Inatumia milisekunde 300 kufunguka (yaani kufumba na kufumbua), mchakato wa kuita usafiri ni haraka na hautumii bando kubwa.
Ramani ya Unakochukuliwa: Uber Lite ina ramani inayomsaidia msafiri wakati wa kuita gari kwa kugundua mahali alipo, kwa hiyo hutakiwi kuandika taarifa nyingi. Ikitokea kwamba haiwezi kugundua mahali ulipo kwa sababu za matatizo ya mfumo wa GPS au kimtandao, inakuelekeza uchague maeneo au mijengo maarufu kama vile Ikulu ya Zamani (jengo ambalo Watanzania wengi hutumia wanapotaka kujua maelekezo ya barabara).
Unabonyeza Badala ya Kuandika: Uber Lite imerahisisha utaratibu wa kuchagua mahali unakoenda kwa kubonyeza tu. Badala ya kuandika mahali unakoenda, unaweza kuchagua eneo lililo karibu na mahali ulipo. Isitoshe, app ya Uber imeweka kumbukumbu ya maeneo maarufu mjini ili maeneo haya yaonekane hata kama huna bando, au wakati hakuna mtandao. Na kadri unavyotumia app ya Uber Lite, ndivyo app hii inavyoboreka. Inajua maeneo unayotembelea sana, na kuyaonesha kwenye app kwanza. Kipengele hiki kitawafaa sana watu wanaotumia simu zenye uwezo mdogo.
Ramani Unapozihitaji: Ili app isichukue nafasi kubwa ya simu yako, ramani haziwekwi kwenye Uber Lite kiotomatiki lakini ukitaka kutumia ramani unabonyeza tu na ramani itaonekana.

Uber Lite itaendelea kutoa huduma na ubora sawa na app ya sasa ya wasafiri, inatoa usaidizi ndani ya app na ina zana muhimu za usalama kama vile Watu Unaowaamini; kipengele kinachowawezesha wasafiri kuonyesha safari yake na wasifu wa dereva kwa marafiki na ndugu kama watano, kipengele hiki kinamsaidia msafiri kumjua dereva na gari analoendesha kabla ya kuabiri gari.

Kufuatia kuzinduliwa kwa app hii nchini Kenya na Afrika Kusini mapema mwaka huu, app ya Uber LITE sasa inapatikana nchini Tanzania na Uganda.

Hivi nidvyo inavyofanya kazi:


Loading...

No comments: