UCHAMBUZI: HATIMAYE ZIDANE AMEMUAMSHA COURTOIS KUTOKA KWENYE NDOTO PORI BY AZIZ MTAMBO - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Thursday, March 21, 2019

UCHAMBUZI: HATIMAYE ZIDANE AMEMUAMSHA COURTOIS KUTOKA KWENYE NDOTO PORI BY AZIZ MTAMBO


Mimi napeda kuita"Ndoto pori" kwa kizungu ni (wild dreams) Ni ndoto aliyokuwa anaendelea kuota kila siku Thibout Courtois, ingawa yeye binafsi aliamini kutimiza lengo la kucheza Real Madrid ilikuwa ni ndoto njema kwake. 

Siku zote, nyasi haziwezi kuwa rangi ya kijani, kuna wakati zinanyauka au kubadilika rangi nyigine yoyote ile. Ni kama maisha yanavyobadilika. 

Courtois hakulijua hilo kabisa. Aliona kuleta dharau na kulazimisha kuondoka, mbele ya mashabiki wa Chelsea, ni faraja kubwa ilimradi lengo la kujiunga na Los Blancos litimie. 

Kweli, alifanikiwa kujiunga lakini akawa anaendelea kuishi kweye ndoto pori bila kujijua. Mbaya zaidi akawa na rekodi mbovu kuliko Klyor Navas. 

Courtois, katika mechi 10, ameshindwa kulinda goli lake lisiguswe. Zidane aliporejea, akaona bado Navas anastahili heshima yake. Kwanin aendelee kumpa nafasi mtu asiye na rekodi za kuvutia? 

Zidane hajasahau mchango wa Navas. Navas alikuwa miongoni mwa watu waliosaidia Real Madrid kushinda makombe matatu ya Ligi ya Mabigwa Ulaya. 

Simaanishi kwamba Courtois ni kipa mbaya hapana, ila anaoneka bora kama safu yake ya ulinzi ni imara. Kama timu iko ovyo na yeye anakuwa mnyonge. Haoyeshi ile nguvu ya kupambana. .

Akiwa Atletico alikuwa bora kwasababu tunajua staili ya Diego Simeone. Ukuta imara kwanza mengine badaye. Pia alipoenda Chelsea bado safu yake ya ulinzi haikumuangusha. .

Hata upande wa timu ya Taifa kweye Kombe la Dunia alikuwa na ukuta imara uliomlinda. 

Tangu msimu huu uanze, Madrid haikuwa kwenye ubora wake. Courtois akawa ovyo pia. Golikipa mzuri ni yule anayeibeba timu yake hata kama haimuungi mkono. 

Kadri siku zinavyoenda, tutaskia Zidane anaruhusu Courtois aondoke ili atafute namba 2 wa Navas. Courtois alipotoka hapendwi, alipo sasa pia hapendwi. 

Kwasasa naona tabasamu limerudi kwa mashabiki wa Real Madrid maana Kylor Navas amerudi kulinda goli. Chelsea wanaendelea kufurahi na kusubiri kuona hatima ya ndoto pori ya Thibout Courtois. 


IMEANDALIWA NA AZIZ MTAMBO.
Loading...

No comments: