UFAFANUZI WA KUHUSU "DEEP STATE" NI NINI, INAUNDWA NA NANI, INAFANYA KAZI GANI NA KIVIPI... - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Wednesday, March 27, 2019

UFAFANUZI WA KUHUSU "DEEP STATE" NI NINI, INAUNDWA NA NANI, INAFANYA KAZI GANI NA KIVIPI...


“Deep State” kwa tafsiri isiyo rasmi ni “Waundaji na Waendeleza Taifa”. Tanzania neno “System” (Mfumo) huwa linatumiwa sana kumaanisha deep state lakini kiuhalisia deep state sio system. System ni mojawapo ya zao dogo tu la deep state na inaweza kusambaratishwa wakati wowote.

Deep State ni kundi lisilo rasmi la kiintelijensia ambalo hujumuisha makundi mbalimbali. Hujumuisha baadhi ya watu waliopo katika utumishi na wastaafu na hata marehemu (maandishi yao) katika intelijensia ya jeshi, usalama wa taifa na hawa huja pamoja si kwa kuambiwa au kuelekezwa bali kwa yale ambayo wao wanayaamini kimapokeo kuwa ni misingi ya uhai wa taifa. 

Watu hawa huamua nani awe mgombea Urais kwa mfano, nani awe Makamu wake, nani awe Waziri Mkuu, nani awe tajiri mkubwa (kwa nchi nyingi za Afrika kwa mfano matajiri wengi wamefanikiwa kwa kupitia kazi za miradi ya umma) kadhalika. Maamuzi haya hayafanywi usiku mmoja, wakati mwingine huchukua miaka wakitumia njia zote zinazowezekana kuhakikisha nani anafikia nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi au sehemu fulani nyeti na nani hafiki.

Wakiamua wewe hutakaa uwe Rais wa nchi kwa mfano, huwezi kuwa. Huwa hawana upendeleo, wana roho ngumu, maamuzi magumu, hakuna anayemzidi mwingine kwa uzito na umuhimu wa maoni na hutazama mustakabali wa nchi kwa miaka mingi mbele, tofauti na wanasiasa ambao wao hutaka tu kushinda chaguzi. Ifahamike kuwa inawezekana hata Rais aliye madarakani asifahamu kwa hakika watu hao wote kwa ujumla wao. 

Hii hutokea hasa katika nchi zinazofanya chaguzi kila baada ya miaka michache. Waasisi wengi wa mataifa huwa ni sehemu ya deep state mfano Mwalimu Nyerere ambaye maandiko yake ndicho chanzo cha Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kufungwa gerezani na hadi leo kuendelea kuota ndoto za kuwa Rais wa Zanzibar ambazo huenda anakwenda nazo kaburini. Deep state huwa ni kama jini, wakati mwingine unaweza kusema halipo ni maneno tu.

Deep state huweza kutikisa nchi kwa kuuhujumu uongozi ulio madarakani kama ikidhihirika walikosea katika kumpitisha kiongozi husika au wakipoteza nguzo inayowalinda ambayo ni uhai wa taifa. Nchini Tanzania kundi la “deep state” halizidi watu 50 katika wakati wowote. 


CHANZO: MEDIUM.COM
Loading...

No comments: