Uganda Watuma Salamu kwa Taifa Stars - MWANAHARAKATI MZALENDO ™

Breaking

Saturday, March 23, 2019

Uganda Watuma Salamu kwa Taifa Stars


Uganda Watuma Salamu kwa Taifa Stars

Timu ya taifa ya Uganda wameweka wazi kuwa wamepanga kumaliza vizuri hatua ya makundi, kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019, ambapo watacheza na Tanzania Jumapili hii.

Uganda ambao tayari wameshafuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Misri, wamesisitiza kuwa wanataka kumaliza vizuri wakiwa juu ya kundi L.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa timu ya taifa ya Uganda, (Uganda the Cranes), wameeleza nia yao ya kushinda mchezo wa mwisho. ''Tuonyeshe uwezo wa juu zaidi katika kumaliza hii hatua'', wameandika. 

No comments: